Israeli: Moto Mkubwa wa Msitu Waua 42
Moto wa siku nne uligharimu maisha ya watu 42, na kusababisha uhamishaji wa watu 17,000 na kuharibu karibu ekari 12,500 kaskazini mwa Israeli.
Ikiielezea kama "moto mbaya zaidi katika historia ya Israeli," Reuters ilisema taifa hilo"lilijitahidi kudhibiti moto mkubwa na mbaya wa msitu... licha ya juhudi za ndege za kuzima moto kutoka nchi nusu dazeni."
Mamlaka ilisema moto huo, ambao sasa umezimwa, ulitokana na uzembe. Gazeti la Jewish Chronicle liliripoti kwamba mvulana mwenye umri wa miaka 14 "alikiri kutupa makaa ya mawe yaliyowashwa, yaliyotumiwa kuvuta bomba la maji [tumbaku], katika eneo la wazi. Wachunguzi wanaamini hii ndio iliyosababisha moto huo mkali, ingawa hali ya hewa kavu isiyo ya msimu na upepo mkali umelaumiwa kwa nini ulienea.
Kati ya wale "waliouawa katika moto mkubwa ulioanza katika Safu ya Milima ya Karmeli... 36 walikuwa walinzi wakielekea Gereza la Damun kusaidia na uokoaji, na waliuawa wakati moto uliokuwa ukienda kwa kasi ulipokumba basi lao moto," gazeti la Jerusalem Post liliripoti.
Afisa wa polisi wa wa ngazi ya juu pia alikufa kutokana na majeraha aliyopata baada ya gari lake la doria kunaswa kwenye msitu unaowaka.


